17.6.2019
saat

All Language

Ikhilas na Taqwa

     Maisha ya mwanadamu hutumika kwa hali moja au nyingine, jambo muhimu ni jinsi gani yanatumika, aidha yatumike katika uchamungu yawe ya Ikhlas kwake au yatumike katika ujahili na yasiwe na maana yoyote.Taqwa ni kule kuyadhibiti matamanio ya kimwili na kuimarisha nguvu ya kiroho kwa binadamu.Hivyo Taqwa huhitajika katika kila eneo la maisha, katika imani, ibada, mahusiano yetu na wengine na hata katika kila pumzi ya uhai wetu. Mafanikio ni jambo ambalo kila mmoja wetu anahitajia kupata. Allah anasema Kwa hakika amefaulu aliyeitakasa nafsi yake, (Ala, 87:14).


Othman Nuri Topbash
ISBN: 978-9944-83-683-8

††

Siri katika upendo wa Mungu

     Mwenyezi Mungu Mtukufu aliujalia uhai kwa siri pekee: Ameuumba kutokana na upendo. Kwa sababu hiyo, kuna upungufu popote ambapo upendo haupo na kuna alama za ukamilifu popote upendo ulipo. Ndio maana njia pekee kwa binadamu kufikia radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu na uombezi wa Mtume (s.a.w) - na hivyo kupata wokovu katika dunia hii na Akhera - ni ukweli rahisi ulio ndani ya siri ya upendo. mwandishi Othman Nuuri Topbash ameuelezea ukweli huu katika kitabu hiki, wale wenye kuujua ukweli huu wakatii maagizo yake hupata hisia kali katika nyoyo zao, Allah atujaalie miongoni mwa walioujua ukweli huo. Na kuifuata njia iliyonyooka.


Othman Nuri Topbash
ISBN: 978-9944-83-692-0

††

  1. Page :
  2. |
  3. 1
  4. |
  5. 2
  6. |
  7. 3
  8. |
  9. 4
STATISTICS :    Total number of languages : 53    Total number of materials : 1.457    Total number of downloads : 1.229.744      ALL STATISTIC 

Coded by IBB SOFT