Tujifunze Uislamu (Kidato Cha Nne)

Himidi zote ni za Mola wetu aliyetupa heshima na furaha ya kuishi kama Waislamu!
Salama nyingi zimuendee kipenzi chetu Mtume Muhammad (s.a.w), familia yake na maswahaba zake walioishi na kuufundisha Uislamu kwa namna iliyokua bora kabisa!
Ni matumaini yetu kuwa tunaweza kujifunza dini yetu nzuri kwa namna bora kabisa, na kuwa miongoni mwa Waislamu ambao Mtume aliyebarikiwa atatabasamu pindi atakapowaona huko Akhera.
Tunamuomba Allah Kupitia mada za kitabu hiki cha “TUJIFUNZE UISLAMU KIDATO CHA NNE” ajaze imani katika nyoyo zenu, aujaze Uislamu katika maisha yenu, na roho zenu azijaze usafi wa moyo. Malaika wasuhubiane nanyi, na watu wema wawe marafiki zenu!


Read In Other Languages

ALBANIAN
ENGLISH