Tujifunze Uislamu (Kidato Cha Tatu)

Himidi zote ni za Mola wetu aliyetupa heshima na furaha ya kuishi kama Waislamu!
Salama nyingi zimuendee kipenzi chetu Mtume Muhammad (s.a.w), familia yake na maswahaba zake walioishi na kuufundisha Uislamu kwa namna iliyokua bora kabisa!
Mtume wetu Mpendwa (s.a.w), alikuwa mwalimu adhimu kabisa aliyefundisha Uislamu kwa wanadamu.
Mtume huyo aliyebarikiwa, aliisoma na kuifafanua Qur’an. Na alitekeleza imani, matendo ya ibada na maadili yaliyofundishwa na Qur’an kwa namna nzuri kabisa. Baada yake, Maswahaba, shakhsia adhimu kabisa wa Uislamu na watangulizi wetu walifanya juhudi kubwa katika kuitekeleza dini hii adhimu na kuipeleka kwa vizazi vya baadaye. Na sasa, ni zamu yetu kujifunza kupitia kitabu hichi cha “TUJIFUNZE UISLMU KIDATO CHA TATU”


Read In Other Languages

ALBANIAN
ENGLISH