Mtume Wangu Kipenzi Mfano Bora wa Kuigwa

Inasemekana kwamba sisi sote tuna jambo ambalo lintuunganisha na Mtume (S.A.W) katika masuala ya kiimani. Katika miili yetu kuna sehemu inayofanana na uzuri wa mtume. Hii ni neema ilioje? Si ndio?
Unafikiri ni sehemu gani ya mwili wako inafanana na ya mtume wetu? Fikiria kuhusu sehemu hiyo… Je, ni macho yako? ngozi yako? au meno yako?
Kwa hakika katika miili yetu kuna sehemu inayofanana na mtume (S.A.W)
Kitabu hiki kinaelezea sehemu ya maisha ya  Bwana Mtume (S.A.W), Kitawapa watoto wetu wa shule ya msingi wenye umri kati ya miaka 6-10 fursa ya kumjua Mtume wetu zaidi.
Kwa kitabu hiki, watoto wetu watamchukua bwana wetu kama kielelezo cha kuigwa na kitawanufaisha katika kukabiliana na matatizo yanayowakabili maishani mwao. Haya tusome!


Read In Other Languages

ARABIC
ENGLISH
FRENCH
RUSSIAN