Naipenda Dini Yangu ya “Kiislamu” - 2
Wanafunzi wapendwa na ndugu walimu:
Tumewatayarishia kitabu kwa jina la “Naipenda dini yangu ya Uislamu” ambacho kitatufunza kuhusu dini yetu ya Uislamu kwa njia ya hadithi, tafakuri na michezo mbalimbali.
Tumekusudia kuwapa wanafunzi wetu fursa ya kusoma kitabu hiki kwa njia ya kufurahisha na kuwawezesha walimu wetu kufanya shughuli ya ufundishaji kwa kuwashirikisha wanafunzi wao. Tunaamini lengo letu limefanikiwa. Hata hivyo, ninyi ndio mtakaotoa tathmini ya mwisho kuhusu kitabu hiki.
Sura ya kwanza inakusudia kuwawezesha wanafunzi kumfahamu zaidi Mwenyezi Mungu mtukufu na Mtume wetu (s.a.w) na dini yetu nzuri ya Uislamu.
Sura ya pili inahusisha shughuli na michezo mbalimbali. Kwa kutumia shughuli na michezo hiyo mtabaini njia bora za kufanya ibada katika dini yetu.
Katika sehemu ya tatu, tutajifunza kuhusu maadili na tabia njema zitakazotufanya tuingie peponi. Tutajifunza pia namna bora ya kuwa na maadili na tabia njema.