Maneno ya mtume (s.a.w) yanaitwa hadithi. Mtume wetu mpendwa alituletea Qur an au maamrisho ya M/mungu. Alitufafanulia maamrisho haya kupitia hadithi zake.Kupitia maneno yake alitufundisha yale tunayohitajika kuyafanya ili tuwe wenye furaha katika maisha haya na kesho akhera.Tunatakiwa kuyasoma mara kwa mara maneno ya mtume s.a.w. Ninafahamu kuwa wengi wanapenda kusoma visa hivyo nami nimekuletea hadithi arobaini sambamba na visa mbalimbali vyenye kutufunza mbao ya dini yetu.