ust_diller

All Language

Historia Ya Uislamu

    HISTORIA YA UISLAMU  imefundishwa mara nyingi na maisha ya mtume wetu mpwendwa (s.a.w) pia  yameelezewa kwa kila namna. Nasi tunawajibika kuwapa Watoto wetu urithi wa kiroho na maadili kwa kujifunza mambo muhimu ambayo yanajumuisha tamaduni na maadili ya kiislamu.
    Hii ndio sababu kitabu hiki kimeandikwa kwa kuelezea maisha na uzoefu wa watangulizi wetu wa utukufu.
    Kitabu hiki kinaelezea maisha ya Nabii wetu mpendwa(S.a.w) na moja ya zama  iliyoongozwa vyema na kwenda Dola ya wauthmanıya (Ottoman Empire). Utapata maswali mengi na njia maalumu za kufundishia ili kuwasaidia wanafunzi kuwa na maarifa zaidi juu ya mada hii ya “HISTORIA YA UISLAMU”.


Kommissionen
ISBN: 978-6053-02-368-5

  

Tujifunze Uislamu (Kidato Cha Kwanza)

     Mtume wetu Mpendwa (rehma na amani ziwe juu yake), alikuwa mwalimu adhimu kabisa aliyefundisha Uislamu kwa wanadamu. Kitabu alichofundisha ni Qur’an Tukufu, muujiza usiomithilika. Nasi Tujifunze Uislamu.


Kommissionen
ISBN: 978-6053-02-240-4

  

Tujifunze Uislamu (Kidato Cha Pili)

     Himidi zote ni za Mola wetu aliyetupa heshima na furaha ya kuishi kama Waislamu!
     Kıtabu cha “Tujifunze Uislamu” kimeandaliwa kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa ngazi ya Sekondari.


Kommissionen
ISBN: 978-6053-02-274-9

  

Tujifunze Uislamu (Kidato Cha Tatu)

    Himidi zote ni za Mola wetu aliyetupa heshima na furaha ya kuishi kama Waislamu!
Salama nyingi zimuendee kipenzi chetu Mtume Muhammad (s.a.w), familia yake na maswahaba zake walioishi na kuufundisha Uislamu kwa namna iliyokua bora kabisa!
   Mtume wetu Mpendwa (s.a.w), alikuwa mwalimu adhimu kabisa aliyefundisha Uislamu kwa wanadamu.
    Mtume huyo aliyebarikiwa, aliisoma na kuifafanua Qur’an. Na alitekeleza imani, matendo ya ibada na maadili yaliyofundishwa na Qur’an kwa namna nzuri kabisa. Baada yake, Maswahaba, shakhsia adhimu kabisa wa Uislamu na watangulizi wetu walifanya juhudi kubwa katika kuitekeleza dini hii adhimu na kuipeleka kwa vizazi vya baadaye. Na sasa, ni zamu yetu kujifunza kupitia kitabu hichi cha “TUJIFUNZE UISLMU KIDATO CHA TATU”


Kommissionen
ISBN: 978-6053-02-447-7

  

Tujifunze Uislamu (Kidato Cha Nne)

    Himidi zote ni za Mola wetu aliyetupa heshima na furaha ya kuishi kama Waislamu!
Salama nyingi zimuendee kipenzi chetu Mtume Muhammad (s.a.w), familia yake na maswahaba zake walioishi na kuufundisha Uislamu kwa namna iliyokua bora kabisa!
    Ni matumaini yetu kuwa tunaweza kujifunza dini yetu nzuri kwa namna bora kabisa, na kuwa miongoni mwa Waislamu ambao Mtume aliyebarikiwa atatabasamu pindi atakapowaona huko Akhera.
    Tunamuomba Allah Kupitia mada za kitabu hiki cha “TUJIFUNZE UISLAMU KIDATO CHA NNE” ajaze imani katika nyoyo zenu, aujaze Uislamu katika maisha yenu, na roho zenu azijaze usafi wa moyo. Malaika wasuhubiane nanyi, na watu wema wawe marafiki zenu!


Kommissionen
ISBN: 978-6053-02-508-5

  

Mama Na Malezi Ya Mtoto

    Kumtambuwa Muumba na kufuata maamrisho Yake ndicho kinachompa thamani mwanadamu. Afya, utulivu na furaha huja katika namna hiyo hiyo tunapotowa huduma kwa binadamu, tunapaswa kulenga kupata radhi za Allah Mtukufu.
    Sisi kama wanawake vijana, tunajifunza kuhusu taji la kuwa mama kutoka ndani ya Qur’an na Sunnah. Kama ambavyo tunajifunza kila kitu kuhusu maisha, vivyo hivyo tunajifunza kuhusu malezi na kuwa mama kutoka ndani ya chanzo hicho hicho. Hivyo, baada ya kujua namna ya kuwa waja wa Allah Mtukufu, hatupaswi kuacha kumuomba msaada wakati tukiwalea watoto wetu.
    Amani na Salamu ziwe juu ya mama wa Mtume wetu kipenzi(s.a.w) na wakeze, ambao ni mama zetu. Amani na salamu pia ziende kwa mama ambao walikufa kishahidi. Mwisho lakini sio kwa umuhimu, salamu maalumu ziende kwa yule ambaye alipitiya maumivu makali katika kuwa njia ya mimi kuja hapa duniani na akanilea kwa nguvu na jitihada kubwa, mama yangu wa thamani, Emine DEMIR. Kila watakaosoma kitabu hiki kwa upendo na hamasa wapate baraka za dua za mama zao na kuwaombea wengine kuwa mama wema. Amiin!!!.  


Neslihan Nur Türk
ISBN: 978-6053-02-842-0

  

Sımulızı Ya Fılımbı Ya Mwanzı

     Nai  (filimbi) iliyotajwa katika  simulizi za Rumi, kiuhalisia, inamwakilisha mwanada mu aliyekamilika (insaan-i kaamil). Hatua ambazo filimbi huzipitia kuanzia kwenye hatua ya kumea mpaka kuwa nai kamili huelezea vizuri kukomaa kwa mwanadamu, yaani hatua hizo ni kielelezo cha hatua ambazo mwanadamu huzipitia katika kuitakasa nafsi na kuung’arisha moyo wake.


Othman Nuri Topbash
ISBN: 978-9944-83-667-8

  

Hijjah Mabrur na Umrah

     Hijja ni kuyabadilisha maisha haya kwa matendo mema na hutumika kutoa ahadi kwa Mwenyezi Mungu ya kudumisha mazuri yanayopatikana wakati wa hijja pindi unaporudi nyumbani kutoka kwenye maeneo haya matakatifu.


Othman Nuri Topbash
ISBN: 978-9944-83-690-6

  

Uıslamu

     Kitabu hiki kinatoa muhstasari kuhusu Uisla­mu. Muhtasari huu ni kama tone la maji ya bahari. Uislamu utakapochunguzwa kwa kina, uta­jitokeza wazi kuwa una mambo mengi ma­zuri ya kutoa. Kwa bahati mbaya, katika zama zetu, kwa makusudi au bila makusudi, Uislamu una­fundishwa katika namna isiyokuwa sahihi na mazuri yake kufunikwa. Lakini, kila mtu mwenye akili, anaweza kuisahihisha akili yake kuhusu Uislamu baada ya kupata picha kamili kutoka kwenye vyanzo sahihi, ambavyo ni vyanzo visivyokuwa na upendeleo wala chuki.


Dkt. Murat Kaya
ISBN: 978-9944-83-686-9

  

  1. Page :
  2. |
  3. 1
  4. |
  5. 2
  6. |
  7. 3
  8. |
  9. 4
STATISTICS :    Total number of languages : 58    Total number of materials : 1.610    Total number of downloads : 2.343.457      ALL STATISTIC

Coded by ibbsoft