Kitabu hiki kinatoa muhstasari kuhusu Uislamu. Muhtasari huu ni kama tone la maji ya bahari. Uislamu utakapochunguzwa kwa kina, utajitokeza wazi kuwa una mambo mengi mazuri ya kutoa. Kwa bahati mbaya, katika zama zetu, kwa makusudi au bila makusudi, Uislamu unafundishwa katika namna isiyokuwa sahihi na mazuri yake kufunikwa. Lakini, kila mtu mwenye akili, anaweza kuisahihisha akili yake kuhusu Uislamu baada ya kupata picha kamili kutoka kwenye vyanzo sahihi, ambavyo ni vyanzo visivyokuwa na upendeleo wala chuki.