Maisha ya mwanadamu hutumika kwa hali moja au nyingine, jambo muhimu ni jinsi gani yanatumika, aidha yatumike katika uchamungu yawe ya Ikhlas kwake au yatumike katika ujahili na yasiwe na maana yoyote.Taqwa ni kule kuyadhibiti matamanio ya kimwili na kuimarisha nguvu ya kiroho kwa binadamu.Hivyo Taqwa huhitajika katika kila eneo la maisha, katika imani, ibada, mahusiano yetu na wengine na hata katika kila pumzi ya uhai wetu. Mafanikio ni jambo ambalo kila mmoja wetu anahitajia kupata. Allah anasema Kwa hakika amefaulu aliyeitakasa nafsi yake, (Ala, 87:14).